PLZ help!!


JAMANI WADAU NAOMBENI MSAADA WENU WA KUNIAMBIA NINI NIPAKE AU NINI NIFANYE KATIKA NYWELE ZANGU KWANI TOKA MWEZI ULIOPITA NIMEONA NYWELE ZANGU ZIMEPUNYUKA, NIKAULIZA WATU WENGI WAKANIAMBIA KWA AJILI YA KUNYONYESHA

NAMI NAAMINI SABABU SINA HISTORIA YA KUKATIKA NYWELE

HIVYO BASI ANAYEJUA MAFUTA GANI NIPAKE ILI NYWELE ZANGU ZIRUDI AU NDO NIKANYOE TU KIPARA NIANZE UPYA , NA KAMA HILO TATIZO ZINAPUNYUKA KUTOKANA NA KUNYONYESHA, JE ITAENDELEA KWA MUDA GANI, KAMA NTAWEZA VUMILIA

SHUKRAN....TUSHEE HAPA KWA FAIDA YA WADAU WOTE

MAMA IQRA
KUNA WADAU WAMEPENDA ONA NYWELE ZANGU B4 HAZIJAPUNYUKA


sehemu zilipoathirika
HAPA NIKIWA NIMEZIJAlADIA!!...Utanijua???!!

37 comments:

Anonymous said...

hi mama Iqra much love kwako na baby wetu.
kwanza pole na maswaiba hayo ya kukatika nywele . hizo ni kati ya changamoto za kuwa mzazi.

kwa kitaalamu mara nyingi hilo ni tatizo linalotokana na kupungua kwa madini hasa ya calcium na mengineyo kwa kuwa madini mengi huwa yanakwenda kwa mtoto kwa njia ya maziwa. so nakushauri ule vyakula vya kuongeza vitamini na madini si wakati wa diet kama unanyonyesha. kuna suppliment unaweza kunywa zitakusaida kupunguza tatizo.
bupe

Anonymous said...

hehehehe we shamim unavisa..eti umezijaladia. wala hujulikani mwenzangu...well kwa mtazamo wangu mimi kweli naona ni kwa ajili ya kunyonyesha. ila itafikia kipindi zitarudi. ila usiache treatment unazotumia kama kawaida. hata mimi nilikuwa namanywele mengi sana kama sophy alivyokwambia...ila nilivyokuwa nanyonyesha zilikatika kama wewe ...sikutumia kitu zikaja kurudi baadae. kwa upande wangu sijajua nini utumie , ila ushauri ni endeleza na treatment kama kawaida yako . zitakaa sawa . usianze kutumia michemical wakati unamtoto mdogo plss. ni ushauri tu mamy...
ur lovely one hawa mkamba.

Anonymous said...

Hili linatokana na dawa unayoweka labda wametengeneza feki. ila kwa ushauri nakushauri sawazisa za juu zenye dawa kisha suka kwa miezi sita na kuendelea alafu uje uweke dawa ya nywele tena tafuta original. labda utuambie unapaka dawa gani?

Anonymous said...

mambo. pole. kweli na mi ilinitokea, ila ule maparachichi kwa wingi na kupaka kwenye nywele ziwe strong. ukiacha zitaacha ila inabidi kuzifanya strong tu kwa sasa. pia ule balance diet unajua maziwa ya mtoto yanafyonza vitu vizuri vyote unavyokula sasa kama unakula machips umekwama.kunywa supu kali,matunda yani maziwa yakifyonza yanabakiza na akiba.

Anonymous said...

Pole mama mtoto. Ndio ulezi huo. Jitahidi usizibane sana nyuma. Na kama utazibana basi jaladia kama ulivyofanya. Ushauri wangu ni kwamba ujitahidi kuzusuka ndogo ndogo na utafute mawigi mawli matatu ya mitoko wakati nywele zako zinakua. Pia mara 1 au 2 kwa wiki paka viks hizo sehemu zilizonyonyoka. Viks inasaidia kuotesha nywele pia.

Anonymous said...

mama iqra,
pole kwa tatizo hilo, ila mm naisi kwa upande wangu kwanza usiwe unasuka zile nywele wanazopenda kusuka wamasai achana nazo kabisa, coz wanakua wanavuta sana na ss nywele za mbele ni nyepesi sana so zinakatika kwenda mbele, pili mafuta ya nazi ni mazuri ingawaje yana harufu kali lkn ni mazuri sana na tatu ikiwa utaweza as u say nyoa para kabisa then uwe unatumia mafuta ya nazi ok.
take ma advise if possible.

Anonymous said...

dah pole.ila jaribu palmers hair success.ni mazuri sana sana sana.la pili pls tuwekee picha ya mwanetu jamani tuna mmisss.plssssssssssssss

Shosticious Lizzie said...

Pole sana mama Iqra ila nakushauri kuna mafuta yanaitwa GRO AID yanauzwa S H Amon au duka moja linaitwa Price pale City Centre ni mazuri sana na huwa mara nyingi yanakuwa adimu but Im sure S H Amon hata ile ya kariakoo unaweza yakuta nilimshauri shostisho wangu alitokewa na tatizo kama la kwako yeye alinyonyoka kwenye kichogo cha nyuma nywele zote aliyatumia yali kwa kweli sasa ana nywele nzuri na ndio mafuta yake....kwa wote wenye matatizo ya nywele nawashauri hayo mafuta pia steaming tumien product ya olive oil ni nzuri sana pia kuweni makini na shampoo za masalon na maji wanayotumia yanakata sana nywele za watu for safe nunua treatment zako na unaweza oshea nywele zako home na maji masafi ya uvuguvugu na kwenda saloon....thanks shosticious Lizzie..

Anonymous said...

pole msweetie!
ila ni kawaida tu kama unanyonyesha, hata mimi nanyonyesha na zilikatika mbele ila sio saana ila hizo kidogo zilizoondoka walionizidi umri waliniambia ni kwa sababu ya kunyonyesha ila mi nilizikata zote nikaanza upya na sasa zimejaa kama kawaida na kwakuwa mtoto anavyozidi kukua anapunguza speed ya kunyonya.naungana na anony mmoja aliyesema maziwa ya mtoto yanafyonza kila vitamin ni kweli kabisaaaaaa tena kuna madini yanayosaidia ukuaji wanywele na uimara wake ndo vyoeete vinaondoka na maziwa vinaenda kwa iqraaaa ndo mana wazazi tunashauriwa kula vizuri kipindi cha unyonyeshaji ukishangaa unaona toto linakuwa bongee we unazidi kukondeana so nakushauri uzipunguze kidogo au uvae mawigi mpaka zilingane (i hope mawigi yanakupendeza),sikushauri usuke maana kusuka sana kunapelekea nywele kukatika especially mbele halafu pendelea steaming za jadi kama hinna maparachichi,maziwa na mayai zitakuwa bomba tena ngumu haswaa.

naima said...

Hi,pole mpenzi hiyo inatokana na kujifungua kwani wewe sasa ure not the same tayari umesha mpa uhai kiumbe kingine so umegawana nacho kila kitu ulicho nacho mwilini kwako,na homon zako pia zimebadilika unacho takiwa kufanya wala usile mavidonge u still young wewe kula venge,fruts,na maziwa sana kwani maziwa ni mazuri sana kwa sie akina dada yana a lot of calcium na usisuke endelea na ratiba yako ya salon kma kawaida na usipende sana kuzifunika kwani pia joto linakata nywele,usiziwaze sana zitarudi tu bila shaka jifanye kma huzioni vile,ni hayo tu msalimie babe wetu we love her a lot.

Anonymous said...

Hellow shamim mimi nakushauri na ipo siku utanishukuru ukinijaribu ukafanikiwa najua utaomba msaada aliyekwambia haya mafuta yanaitwa Aba Soda mpenzi hiko kipara kitakuwa kam wayataka nenda kariakoo yale maduka yanauza vitu vya kienyeji karibu na stand za mabus ya Mwenge au kam wamjua mtu akuletee toka Zanzibara ni Meusi kiukweli hata mimi waz Mzazi mwaka 2007 yalinisaidia kinoma nayaaminia ni noma ila Please ukifanikiwa Find me kushukuru kiukweli utayapenda hair zitajaa ila uache kushonea weaving au kusuka na rasat wewe kuwa buzz na hayo mafuta waweza Mix na unayotumia.All da besty shabiki wako wa blogger kiss little angle Iqra

Anonymous said...

mimi ninauhakika nikunyonyesha kwasababu imenitokea sana kukatika nywele ni kwasababu ya kunyonyesha tu na wala hakuna kitu kingine wewe endelea na steming ya mayonise uwe una zi seti walau mara moja kwa wiki basi inatosha usijihangaishe na kitu kingine kama huamini ukija kuzaa mtoto mwingine utaona ni hivyohivyo utakuwa mzoefu.utajua chakufanya.mimi nina watoto na nilikua hivyo na nilifanya hivyo zikarudi.zinarudi tu tena zinakua ndefum kuzidi hata mwanzo .amini na jari bu kuuliza watu wenye watoto watakwambia asiye na mtoto hawezi kukuelewa maana haijamtokea inakua ngumu kujua.mdau fin

Anonymous said...

He sikujua kumbe kunyonyesha kuna shughuli asanteni sana wadau mmenifumbua leo, mie mjamzito na nna nywele ndefu zimeshiba ila sasa i know what to expect. wadau endeleeni kumshauri na sie kina fulani tupate shule ikifika wakati wa kunyonyesha tujue haswa cha kufanya

pam said...

mmmh tiba ni kula balancing diet tu na ku pause hadi kipindi kipite zitakuwa in its normal condition zenyewe...mimba au kunyonyesha ni very funy kipindi wengine huumwa na meno balaa usipokuwa makini utayapeleka kun'goa kumbe ni upungufu wa calcium and iron kwani kipindi hiko mtoto anakupokonya kinoma...thats why wanasema maini dagaa ni muhimu.mimba ikipita meno yote yamepona haya ungeng'oa?teh teh teh.

Anonymous said...

Hi Zeze,
Pole sana kwa tatizo hilo. Kuna mafuta ya nywele special kwa ajili ya tatizo hilo. Ni product ya UK na yanapatika Dar kwa some agent. Kwa maelezo zaidi jinsi ya kupata mafuta hayo wasiliana na Agent kwa mob no 0784-534312. Nitakutumia website ya hiyo product for more information.

Anonymous said...

Jamani me mwenzenu naona kama imenitokea kivingine sijui nikoje? me wakati wa mimba sikuwa na nywele, na nilipojifungua wakati wa kunyonyesha ndo nikawa na minywele rundo yani watu walishangaa kuniona na nywele vile, sasa nilipomuachisha mtoto baada ya mwaka mmoja na miezi 4 ndipo nywele zikaanza kunyonyoka..sikuelewa ila nilishauriwa nitumie hiyo Palmers hair success ndo zikaja kurudi.

Mamuu

Anonymous said...

ni kunyonyesha tu mpenzi,hata mimi zilitoka sana ila usiwe na wasiwasi zitakuwa tu ok as time goes by...the joy of having and seeing your baby everyday outweighs watever comes with it.much love

Emma said...

zeze mi ni mdau niliyekuahidi kukupa website ya mafuta ya kurepair nywele hasa matatizo kama yako and many more for massive hair growth yanaitwa T444Z hair food cash back quarantee hair product. tena kwa mtu mwenye nywele kama zako ukiyatumia properly utaona matokeo ndani ya mwezi mmoja. Mimi nilishatumia gro aid, hair success na mengine mengi lakini tangu niweintroduced na T444Z ninayatumia miaka miwili sasa nywele zangu ziko very healthy and long than before. Ni mafuta special kwa ajili ya natural na relaxed hair na safe kwa watoto kwani hayana chemicals yanatengezwa na natural stuff only. Jionee mwenyewe kwenye www.t444z.com upande wa kushoto kunasehemu ya profile ambayo mwanzilishi wa mafuta anawafuatilia watumiaji wa mafuta hayo before and after. hizo ni picha za kweli na baadhi ya watu kwenye picha nawafahamu.
haya wadau mafuta hayo yako dar kazi kwenu mwenye kuhitaji namba ya kupiga ni 0784534312 mwanamke nywele

Anonymous said...

ahh mamuu bila shaka ulikuwa unatoka pasu na mtoto, he hee kakigoma ahh mama unamalizia

Anonymous said...

Hey, mama Iqra ni kweli kunyonyesha kunasababisha hivyo kutokana na "hormonal imbalances". Ila pia na madawa ya nywele unayoweka, solution ni kuzipumzisha kwa muda labda usuke kidogo. Ule vizuri matunda, mbogamboga na protein kwa wingii!!!!Pia WEAVING inachangia kukatika kwa nywele....
Goodluck!!
Mama Ushauri

Anonymous said...

acha kukaa na nywele zilizosukwa kwa rasta kwa muda mrefu sana na pia weaving wakati wa kulichana unakuwa unavuta zile nywele kwa nyuma so jitahid pia usikae nalo sana,ujitahidi kuzifanyia treatment i mean steaming mara kwa mara.

mdau nrb.

Anonymous said...

Shoga kidawa hakuna mafuta kata zote (sio kipara pls) nunua lace front (usiweke gundi) subiri ziote upya. thats it..

Anonymous said...

My dear pole..Unaweza ukawa unapaka SUNSILK DAMAGE REPAIR ni ya maji very nice me nywele zangu ziliharibika sana kwa rangi now ziko sawa ni sh elfu saba mpaka kumi unaweza nunua na shampoo na conditioner yake zinapatikana in different cosmetic shops in Dar.. halafu pia nimeshawahi kuambiwa Habasoda inasaidia pia kustimulate growth..Habasoda i thnk unaweza pata hata kkoo kwene yale maduka ya spices..Unakua unaisugua kwene affected area..

All the best..Mamu(Dar)

Anonymous said...

Zeze mumy sasa hivi kata hizo nywele,,halafu usipake dawa yoyote wewe kula mitindo tu ya kusuka kichwani mpaka umalize shughuli ya kunyonyesha,, mimi yalinikuta nilifanya kama nilivyokushauri,,umama kazi mdogo wangu na kulea ndio kazi kabisa,,

ila naomba unifikishie salamu kwa huyo Hawa Mkamba, sijui niyule aliyesoma Mtendeni primaly school??
mwambie mimi ni Monica Daffa,, tulisoma darasa moja,,
shukurani SHAMIM

Anonymous said...

My Dear Shamim a.k.a.mama Iqra a.k.a ZEZE tumia Dr Miracle`s anti-breakage strenghtening cream yapatikana pale SH Amon ni nzuri sana utashangaa within a month unywele huo bibi kama uyoga!Sawa love kuna product yote shampoo na vikwerombwezo vingine ukipenda!

Anonymous said...

Tumia Dr Miracles shampoo na super gro maximum strength. utaniambia yaani wiki mbili tuu utaona nywele zitakavojaa. mie nilikuwa kama wewe kabisaaaaa nikaona kwenye oprah imekuwa recommended na oprah waga arecomend ovyo yaaani it works kabisaaaaa.

Shadida said...

shamim umzuri tena sana MashaAllah,una uzuri wa kuzaliwa,Mungu akuzidishie.
hata na mimi nilikuwa kama wewe,nywele zote zimenyonyoka mbele.
Mimi ushauri wangu ni hivi kwa sasa bora zikate zote,zitachipuka nyengine mpya,yaani uzikate saizi ya hizo za mbele zilizotoka,hadi utakapomuachisha Iqra na manywele yako yatakuwa tayarikama kawaida tu.
Ila hata hivyo huo utokaji wake pia zimekupendezesha dada.
Mimi nataka unipe siri ya ngozi yako upo soooft MashaAllah.

Anonymous said...

Hao wanao kuambia unatumia dawa zilizopita muda wake, nenda kwa Amon, kula parachichi wote huenda hawana ufahamu juu ya hormone au mabadiliko ya mwanamke baada ya kupata ujauzito na kujifungua, hayo ni mabadiliko ya hormone ktk mwili wako baada ya kupata ujauzito na kujifungua...there is nothing about kunyonyesha kwani dada yangu hanyonyeshi ana fake (bobs) na ana wtoto wa 3 na kila mara akijifungua anakatika nywele balaa...alichoshauriwa ni kutooshanyewle mara kwa mara, ila hakikisha ziwe safi, pia aliambiwa asitumie mafuta yeyete ya nywele (ya mgando) kama blue magic na aina yeyote inayo endana na hiyo, badala yake alishauriwa kutumia (spray) ambayo wengi tunatumia baada ya kuset nywele zetu....nyele zilipungua kukatika mpaka zimekua katika hali nzuri sasa. tchao.

Mwali said...

Sikiliza Mama Iqra....
Usizichoshe nywele zako zaidi kwa kupaka Chochote, mwanao akikua na ukalikisha on time hayo masaibu yote yatakwisha, ni changamoto za kuitwa mama hizo.... ndio maana wengine huwa wanakata kabisaa hasa maana huwa wanabaki na nywele nusu kichwa, we mbona zina afadhali??? wengine wanaamuna kuwanyima watoto wao haki za msingi na kuwalikisha mapema, alafu wakikosa inteligency baadae wanawalaumu....
In short, hakuna cha kupaka zaidi ya kula vizuri na kumnyonyesha vizuuuri mwali huyo!!!!

Anonymous said...

Mambo Zeze! Mimi niliona kwa dada yangu amenyonyesha na nywele zake hazikukatika kwa kuzingatia haya yafuatayo:- Jitahidi kufanyia steaming nywele zako mara 2 kwa wiki na usipende kuzibana au kuziachia mara kwa mara au kuzichana kila wakati ila we jitahidi kuzisuka hizo nywele zako mwenyewe na si yebo yebo coz zitazidi kukatika .... Zingatia hayo na utaniambia halafu funga sana vilemba usilalae bila kilemba. Nafurahi kwa kusoma comment yangu na kuzingatia haya .... It's me 8namba!!

Anonymous said...

me unanitia uchungu....jamani yaani ndio zimeathirika hivyo?! Lakini kusema sababu ya kunyonyesha me nakataa coz mbona wengine hatujanyonyesha hata kidogo lakini nywele zetu ziliathirika tu.

niwael said...

kuwav busy kidogo na nywele zako then upekusuka ili zikuwe.suka za kawaida kama itakuwa ngumu ww kutoka nje hivyo weka wigi juu.baada ya mwezi 2 nenda kaweke dawa na fanyia steaming ya ki2nguu swaumu.jizoeshe hivyo ndani ya miezi 3.naamini utaona mabadiliko makubwa,

Anonymous said...

Shostito Shamimu mambo, pole na majukumu. Achana na product za kemikali hazina lolote. Nenda Posta-IPS building ghorofa ya tisa kuna ofisi za Product of Nature zinatengenezwa na dada mmoja specialist wa kitanzania anaitwa Rose Aziz. atakuelekeza utumie product gani kati ya alizo nazo. Nakuambia utashangaa within three weeks. mimi natumia products zake ambazo ni za asili na zina tbs nimeona manufaa. Please nenda leo utaniambia.

Shostito Ikunda.

Anonymous said...

POLE NA TZTIZO HILO LA KUKATIKA NYWELE.
USHAURI..
NAJUA HII INAWEZA KUWA NGUMU KIDOGO LAKINI FANYA JUU CHINI UTAFUTE MBEGU ZABANGI,ZIGRIND ZIWE KAMA UNGA FLANI HIVI,CHANGANYA KWENYE MAFUTA YOYOTE UNAYOPAKAGA YA NYWELE,PAKA KILA BAADA YA SIKU NNE HIVI ...NYWELE ZAKO ZITAONEKANA CHAFU FLANI HIVI NDO MANA NASEMA USIPAKE KILA SIKU.PAKA KWENYE NGOZI TU.MI NILIKUWA NNA NYWELE CHACHE TANGU NIMEANZA KUTUMIA HIZO MBEGU ZA BANGI ZIMENISAIDIA.

OR

CHUKUA OLIVE OIL KIJIKO KIMOJA,COCONUT OIL KIJIKO,NA ALMOND OIL KIJIKO.PASHA MOTO ULE MCHANGANYIKO.PAKA KWENYE NYWELE BAADA YA KILA MUDA FULANI.INASAIDIA SANA.

JARIBU NA UTAKUJA NAMBIA.

isha said...

AAa mama iqra
pole sana shamim but dont worry kwa ushauri wangu kama mimi, Nywele zako punguza zile level moja, mafuta tumia Dr Miracle`s anti-breakage, na dawa ya nywele weka Iman then utaona habari yk.

Anonymous said...

Hakuna cha kwenda "IPS building ghorofa ya tisa kuna ofisi za Product of Nature zinatengenezwa na dada mmoja specialist" nani mtaalam wa nywele tanzania tusidanganyane...kasomea wapi? ana vyeti adhibitishe? kama hakununua kenye mitandao kwa bei ya jumla na kuwauzia wa wadanganyika kwa reje reja :) :) :)... watakuyeyusha wakuuzie maproduct kibao ambao hata wao hawajawahi kutumia... kama unataka kuwa majaribio ya nywele ndenda...wapo kwa ajili ya biashara na si kusaidia mtu...nenda hapa utapata suluhisho kwa wataalam..www.strengthofnature.com

Anonymous said...

MAMA IQRA NIMECHEKI NA MTANDAO KUHUSIANA NA NYWELE KUNYOFOKA NA HII NDIO SABABU HAPA CHINI>>>>>
INAHUSIANA NA UZAZI LAKINI SIO DIRECT NA KUNYONYESHA..SANA2 NI PART PLAYED NA HORMONES WAKATI WA UJAUZITO NA KUJIFUNGUA>>>>

I had my baby three months ago, and now my hair is starting to fall out. Is this normal?

Many new moms are surprised to find themselves shedding more hair than usual in the first few months after giving birth, but it's perfectly normal. And there's no need to panic: You won't go bald. In fact, your hair should be back to normal by your baby's first birthday.

Here's what's going on. Normally, about 85 to 95 percent of the hair on your head is growing and the other 5 to 15 percent is in a resting stage. After the resting period, this hair falls out — often while you're brushing or shampooing it — and is replaced by new growth. An average woman sheds about 100 hairs a day.

During pregnancy, increased levels of estrogen prolong the growing stage. There are fewer hairs in the resting stage and fewer falling out each day, so you have thicker, more luxuriant tresses.

After you give birth, your estrogen levels take a tumble and a lot more hair follicles enter the resting stage. Soon you'll have more hair coming out in the shower or on the brush. This unusual shedding will taper off and your hair will be back to its pre-pregnancy thickness about six to 12 months after you give birth.

By the way, not all women notice dramatic changes in their hair during pregnancy or the postpartum period. Among those who do, it tends to be more obvious among women with longer hair.