VODACOM FOUNDATION...YAFUNGUA TENA NAMBA YA MAAFA ILI KUSAIDIA GONGOLAMBOTO

 
       Vodacom Foundation kusaidia wahanga wa Gongolamboto

Mkurugenzi wa Mahusiano na Vodacom Foundation Bi Mwamvita Makamba ameviambia vyombo vya habari kwamba
Kampuni yake kupitia  mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation umeguswa na janga la milipuko ya mabomu yaliyotokea  katika kambi ya Jeshi Gongolamboto Jijini Dares Salaam:Na hivyo kumfanya kuamua  maamuzi ya haraka kama  yafuatayo.

1.       Kufungua tena namba yao ya maafa ili kuruhusu watanzania ambao wangependa kuchangia wenzao kufanya hivyo kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15599 kupitia mitandao yote.
Ujumbe huu utatozwa shilingi 1000 na pesa zote zitaenda kwenye tume ya maafa ya serikali ili kuweza kununua vitu vya dharura vya wahanga. Red alert itawasha rasmi kesho ijumaa tarehe 18.

2.       Vodacom Foundation itatoa chakula na vinywaji  kwa  siku nzima ya ijumaa kwa wahanga zaidi ya 1000 waliopo Uwanja wa taifa ambao wengi wao ni watoto
3.       Pia Vodacom foundation imetoa namba za simu kwa timu ya clouds ilioanzisha kituo cha habari na matukio huko shule ya mzambarauni ukonga. Namba hizi zinatumika kupiga bure na kutoa taarifa ya kupotelewa Ndugu au jamaa na pia kutoa taarifa ya maafa zaidi ambayo hayajulikani ili taarifa ziende kwa wahusika. Namba hizi ni 0767 111401 , 0767111402 na 0767111403
4.       Pamoja na kuwawezesha watanzania kutuma mchango wao kupitia ujumbe mfupi, Vodacom Foundation pia unakusanya misaada ya chakula na maji na vifaa mbalimbali katika Ofisi zao zilizopo Mlimani city kwa watu ambao hawajui waipeleke wapi. Misaada hiyo itakabidhiwa kwa red Cross ambao wanahudumia wahanga waliopo Uwanja wa taifa na sehemu  mbalimbali

NAWE KAMA MDAU UNA NAFASI KUUBWA YA KUCHANGIA MAAFA HAYA KWA NAMNA MOJA AU NYENGINE  KWANI WAHANGA HAWA WANAHITAJI DAWA,DAMU VYAKULA
 (vinashauriwa vile vikavu kama biscut,mikate nk ambavyo si vya kupika) PIA ZINAHITAJIKA NGUO (mashuka, kanga nk) BILA KUSAHAU PAMBA KWA KINAMAMA

TAYARI SHEAR ILLUSIONS WAMENIKABIDHI KANGA PEA 20, NAWE KAMA MDAU WA 802 FASHIONS UNA NAFASI YA KUCHANGILI HILI TAFADHALI KAMA UKO MKOANI WAWEZA TUMA UJUMBE KUPITIA NAMBA  15599  ILI KUCHANGIA. WEWE WA DAR ES SALAAM TEMBELEA VITUO  TOFAUTI VINAVYOTANGAZWA KIKIWEMO CHA  UWANJA WA TAIFA NA SHULE YA UKONGA MZAMBARAUNI AU OFISI ZA VODACOM MLIMANI AU OFISI ZA CLOUDS FM AU HATA TUWASILIANE TUJUE JINSI GANI YA KUFIKISHA MSAADA WAKO

MAMA IQ


0 comments:

Post a Comment