MJADALA::KUBADILISHA MATRON


MASHOST LEO HEBU TULIJADILI HILI

Siku za karibuni nimeona Baadhi ya sherehe maharusi wakiwa wamebadili matroni yaani mtu anakuwa na matron wa kitchen Party, Sendoff na wa Ndoa

Hebu mnijuze ni fashion au kuna kitu gani kinatokea hadi kupelekea Bi harusi mmoja kubadili matron kwa kila sherehe na ashindwe chagua mmoja ambaye atamsimamia katika sherehe zote...kama enzi zetu sisi

Na mkumbuke kuna wengine hawana matron katika baadhi ya sherehe kama Send off na Kitchen party... lakini hili TUPA KULE...TULISHALIJADILI


15 comments:

Anonymous said...

Hili ni kweli. Ila mie sababu yangu ilikuwa ni kwamba nina mashoga watatu. Na kila mmoja nilitaka aone kuwa ana umuhimu kwangu. Therefore nikawapa wote chance ya kuwa made of honors.MMoja k/party, wa pili sendoff, na mwingine kwenye harusi.

Anonymous said...

Ili kupunguza gharama na mzigo kwa matroni kununua nguo na viatu mara tatu, kwa maisha ya bongo sio rahisi mtu akaweza kununua vitu vya sherehe tatu kwa mara moja.

Anonymous said...

ni kweli gharama ni kubwa kuwa na matron mmoja tu inategemea na uwezo wake kifedha.

Anonymous said...

availability of the person also matters.

Anonymous said...

na sisitiza hapa kwa matron ni afadhali wangekua wanachukua rangi kidogo inayo ingiliana na mtarajiwa ili isi fanane kila kitu mimi naona kama hapa matroni kapendeza kuzidi biharusi sasa hii sio nzuri angechanganya rangi nyingine kidogo ili kutofautisha sana na mtarajiwa ili iwe siku yake tu sio mtu unatamani sijui umchague nani.na mimi nafikiri kitchen party mtu unakua peke yako send off unachagua eidha uwe na mtu au usiwe nae yote ni ubunifu unatakiwa.mitindo ipo kwa mustafa,naledi,na wengine ukicheki utapata nguo nyingi za kitchen party kila siku nguo kama za send off zina chosha.

Anonymous said...

mamboz wanablog!! mimi napenda kazungumzia kwa upande wa wakristu, utakuta mtu anapenda shoga yake amsimamie kwenye sherehe zake labda zote tatu lakini kwa ndoa inakuwa inashindika labda kama huyo shoga yake hajaolewa so inakuwa ngumu, kwa sababu msimamizi wa harusi kwa baadhi ya makanisa anatakiwa nae awe na ndoa!! so mtu anakuwa ana matron wa send off na k. party na wa harusi mwingine.

Anonymous said...

sometimes matron uliyemchagua kwa kpat hana nafasi ya kuwepo kwenye harusi au Soff kwa either safari za kikazi au kama harusi inafanyika mkoa tofauti na ilipofanyika kpat au Soff. Lingine matron unayemtaka anaweza kuwa hajaolewa hivyo akashindwa kukusimia harusi especially kwa makanisa ambayo hayakubali So unakuta mtu ana matron tofauti.

Anonymous said...

kwa upande wa matron siku harusi ni lazima awe na ndoa, sasa unakuta labda alo tayari kukusimamia siku ya harusi yupo tight si mnajua mambo ya bongo tena, mishe mishe kibao, hawezi kukusimamia siku zote tatu, ndo mana utakuta wengi wanabadilisha ma-matron mana kwenye k/pati na sendoff ndoa si lazima sana, ni kwamba tu upate mtu wa kukupa tafu pale mbele, nadhani kwa kukwepa gharama ndo mana wengine wanaamua kusimama peke yao kwenye k/pati na sendoff, kwenye harusi ndo utakuta yuko na msimamizi, ila inataka moyo...
kuwa peke yako pale mbele

Namkunda said...

Mi naona ni vizuri kubadilisha inakuwa na sura tofauti na zamani tunaenda na wakati na pia inapunguza gharama za nguo na viatu mana kitchen part lazima uonekane tofauti na sendoff hivyo hivyo kwa hiyo wakiwa tofauti inakuwa nafuu zaidi

Anonymous said...

kwa upande wangu sioni umuhimu wa matron kuvaa almost sare na mwenye harusi.

kwa kweli naona haimpi nafasi ya ku-shine biharusi peke yake.

its her day and she should be the center of attention, y think of looking like cinderella when there will be two cinderellas around?

Anonymous said...

bongo si mnasemaga mna hela za kumwaga, sasa kwa nini mnapunguza tena gharama. i am assuming the lady is in bongo, maana maulaya kwenu huko hakunaga shughuli nyingi ivo. ni bridal shower na arusi thats it

Anonymous said...

Ya. Hilo la garama nakubaliana nalo, na hata hilo la kuonyesha umuhimu wa watu pia nakubaliana nalo.

Anonymous said...

mi nadhan kikubwa ni gharama,maisha yanazid kuwa magumu mambo mengi sn siku hzi na hizi shughuli ndo usisemekila mtu anataka mchango

Sidhani kama mtu anapenda kuchukua matrons wtofauti kiasi hicho manake kuna wale unakuta hawajaolewa basi wanasimamia send off na kitchen party, harus inabd kubadilsha lakin ingekuwa inawezekana unaweka huyo huyo

All n all mi nadhani ni kupunguza gharama

Anonymous said...

mh kazi sana, harusi za siku hizi?

Anonymous said...

nafikiri watu wanapoteza maana halizi ya sherehe hizi,
Mimi nasema ukweli mtupu, atakaechukia na achukie tu wala sitajali mradi nimesema.
wote wanaobadilisha wasimamizi, wanachemsha
hakuna cha gharama wala nini, tusipotoshane hapa, matroni anatatakiwa kuwa mmoja tu!, kitcheparty, sendof na hata harusi, sio siku hizi watu wanajibunia tu! utakuta kitchepart mtu anasimamiwa na mtu ambae hata hajaolewa, au unakuta harusi mtu anasimamiwa na wanandoa tofauti, ili iweje sasa?? mh hizi fasion siku hizi ni too much.
INAPENDEZA UKIWA NA MSIMAMIZI MMOJA TU!