JAY DEE AGUSWA NA MJADALA

"Kipensi changu tangu 2003...kauka nikuvae"


Kusema na ukweli mimi binafsi kuna nguo ambazo huwa nazipenda sana na natamani ningekuwa nazivaa kila siku, kuna jeans yangu moja hivi suruali ambayo huwa hai piti wiki sijaivaa.
Na hii ni kutokana kuwa najisikia huru sana kuivaa yenyewe kuliko nguo zingine.

Kitu kingine ambacho mimi hukipenda zaidi ni hiki ki kaptula, ukichanganya na hili joto la bongo huwa nakivaa daily jamani mpaka Gardner ananiita Jide ma jeans. Hii kaptula niliinunua mwaka 2003, na hizi picha ni 2009 / 2010 na bado nakipenda na nitaendelea kukivaa... na kuna picha za 2005 nina hiki ki kaptula sema sikumbuki zilipo nikipata nitawatumia

Najiskia fresh zaidi kuliko nguo nyingine yoyote, na inatokea kwa watu wengi sema hawapendi kuweka mambo wazi........Hata uwe na nguo kiasi gani huwezi kuvaa nguo mara moja usirudie, tusidanganyane...

Mimi zipo nguo inapita miaka sitamani hata kuzivaa zinakaa kama mapambo lakini kama nguo unaipenda na unaona inakufanya uwe huru zaidi utairudia tu.

Ni kweli wanawake / wasichana wa bongo kokote mlipo na mnaotuma hizi comments huwa hamrudii nguo??
Au ndio nyie mkiona camera mnakimbia mpaka mpate nguo mpya, kuweni huru ukizingatia hatuna utajiri huo..

Na ukiwa na mapenzi na kitu, hata uwe navyo vingi kama unapenda kimoja unapenda tuuuuuuuu

JIDE

ALIYEGUSWAAAA?!!!

0 comments:

Post a Comment