UPI UMRI WA KUACHANA NAFASHION?!!

UPI UMRI WA KUACHANA NAFASHION?!!

UPI UMRI WA KUACHANA NA FASHION???

WADAU LEO HEBU TUHABARISHANE UMRI AMBAO FASHIONISTA ATATAKIWA AACHANE NA FASHION, MAANA NIMEKUWA NIKIONA COMMENT HAPA WADAU WANADAI MTU AVAE KUTOKANA NA UMRI JE MNAMAANISHA MIAKA MINGAPI ? NA AVAE NINI ASIVAE NINI?

MIE KWA MTAZAMO WANGU UVAAJI NI HULKA YA MTU, HUWEZI MLAZIMISHA MTU AJIFUNGE KANGA YA MABEGANI KAMA WENGINE WALIVYOZOEA SHINDA NA KANGA, AU AVAE VITENGE ETI KISA YEYE NI MTU MZIMA

COS KUNA WENGINE TUKIVAA SUTI TUNAAMBIWA TUNAJIZEESHA...wink

SIONI AJABU HATA KIDOGO KWA MTU AMBAYE YUKO KWENYE ENTERTAIN MENT AKIFANYA STYLE YOYOTE NAMZUNGUMZIA MWANAMUZIKI, MUIGIZAJI, MWANAMITINDO ,MTANGAZAJI WA VIPINDI VYA BURUDANI NA SI MSOMA HABARI nk .

NITASTAAJABU SAANA MTU KAMA MIE SHAMIM (namaanisha Muandishi wa Habari) MWANASHERIA OFISINI, DAKTARI ,SEKRETARI, MWALIMU,MHASIBU,HR, BANK TELLER NK AKIWA AMEVAA KAMA MTU WA ENTERTAINMENT AKIWA OFISINI

NADHANI MAZINGIRA NA KAZI TUNAZOFANYA ZITAKUONESHA UVAAJI NA SI UMRI , NA PIA JE UMEVAA UNAENDA WAPI, COS HATA WE MWANASHERIA SITEGEMEI KUKUKUTA NA SUTI DISCO UKIULIZWA NINI MIE MWANASHERIA , AU WEWE MWANAMUZIKI NAKUKUTA NA KIMINI CHAKO KANISANI.

BADO NASIMAMIA KWENYE MAZINGIRA ULIOPO NDO YATATOFAUTISHA UVAACHO NA WE MWENYEWE NINI UKO COMFORTABLE NACHO NA KAMWE SI UMRI WA MTU.

NYIE MNAONAJE??

SJP

Naomi Campbell
kylie minogue
vivica fox
Mama yao na Kim Kardashian
Mama Beyonce

hizi picha nilizoweka ni za wanawake ambao ni zaidi ya miaka 40, lakini wanalipuka mbaya na fashion.
je nao wajihuzuru au umri bado????