MUSTAFA AJA NA FASHION FOR HEALTH!!

 

Kampuni inayotoa huduma za simu za mkononi ya Vodacom kwa kupitia Vodacom foundation mwaka huu itadhamini maonyesho ya mavazi ya hisani “Fashion 4 Health Black and Gold Gala” yanayolenga kuboresha hali ya mazingira ya Hospitali ya wenye matatizo ya akili Zanzibar.
 Kwa mara yatatu mfululizo Mustafa Hassanali ataonyesha maonyesho ya mavazi ya hisani yaliyo andaliwa na Explore Zanzibar kuchangia ukarabati wa Hospitali hiyo. “Tukiwa kama wazanzibari tuna jukumu na wajibu wa kuwapatia maisha bora watu hawa ambao wanaonekana kama wametengwa katika jamii”.
Anasema Maryan Olsen mkurugenzi wa Explore Zanzibar. Kwa kumuunga mkono Maryam Olsen,Vodacom Foundation na Mustafa Hassanali wameunganisha nguvu zao pamoja ambazo zitanufaisha wahanga katika hospitali hiyo. ‘Mwaka huu tunataka kurekebisha wodi ya wanaume na kujenga kituo cha michezo ,ni kwa miaka mingi sasa wagonjwa ,wamekua wakikaa tuu kwenye wodi zao bila ya kichocheo / kiburudisho. 
Taratibu lakini kwa uhakika tunalibadilisha hili. ‘Wagonjwa wana kila sababau ya kuishi na kujifunza katika mazingira ya kupendeza . lakini tunahitaji msaada’ alisema Mustafa ambaye kwa Pamoja na Explore Zanzibar wamedhamiria kuboresha maisha ya wagonjwa katika hospitali ya wenye matatizo ya akili Zanzibar iliopo Kidongo chekundu,Zanzibar mjini. 
Mustafa Hassanali mbunifu maarufu atazindua ubunifu wake mpya tarehe 30 Julai 2010. uzinduzi huo utafanyika hoteli ya Zanzibar Serena Inn akiongozana na wanamitindo kutoka Dar-es- salaam. Vilevile mbunifu maarufu mwenye makazi yake visiwani Zanzibar Farouque Abdella atafungua pazia la maonyesho hayo akifuatiwa na mbunifu Mago.
Maonyesho hayo yatapambwa na burudani kutoka kwa Tanzanite Band . Maonyesho hayo ‘Fashion for Health with Vodacom Foundation’ Black and Gold Gala’ yamedhaminiwa na Vodacom Foundation ,PSI(Population service international), Africa Life Assurance ,Explore Zanzibar, 361degrees Events, Vayle springs Ltd and Mustafa Hassanali

0 comments:

Post a Comment