MSAIDIENI HUYUUU

naomba msaada kwa wadau na kwako zeze pia, mimi ni mwanamke ,niliye katika ndoa kwa miaka 6 sasa, na nimebahatika kupata watoto 2 tayari. ila nina tatizo kubwa saana kwenye ndoa yangu, kutokana na kwamba mume wangu amekuwa limbukeni saana wa ,wanawake wa nje wenye makalio makubwa kiasi kwamba mara kwa mara nimekuwa nikimfumania na wanawake wa aina hiyo, lakini aliponichumbia na kunioa alijua kabisaa kuwa mimi nina umbo la kawaida  lakini ghafla alianza kunishawishi nitafute dawa za kuongeza makalio , kiukweli swala hili limekuwa gumu kwangu saana kutokana na maadili  na malezi niliyokulia, ajabu juzi nimemfuma tena na mwanamke mwenye makalio na jibu alilonipa mi mwenyewe nilichoka kwani aliniambia chukua hizi laki 2, nifanye juu chini nipate  dawa za kuongeza  makalio...na kama makalio yangu hayataongezeka kwa miezi miwili basi nijiandae kumpokea mke mwenzangu. shamim nampenda saana mume wangu  siko tayari kabisa kuachwa mungu atanisamehe naomba jamani mnielekeze hizo dawa nitazipataje na zinaitwaje wala msitaje majina yenu ,nielekezeni  tu ili niinusuru ndoa yangu  maana mo mpaka sasa sijapata  hata kazi huyu mume wangu ndio kila kitu kwangu
nisaidieni jamani

0 comments:

Post a Comment