Pata nakala yako ya toleo la 11 la jarida jipya la maswala ya urembo na mitindo ya nywele la Shear Hair & Beauty. Ndani ya toleo hili utapata mambo mengi;
Mjue miss Universe Tanzania Hellen Daunsen msichana mwenye umri mdogo aliyepitia mengi na safari yake iliyomfikisha hapo alipo leo; ushauri kwa wasichana chipukizi kuacha kutumia vipodozi na kujua siri ya kuwa mrembo ni nini; maelekezo ya kujenga mwili kwa kufanya mazoezi ya uzito na umuhimu wake kwa afya ya mwanamke; jinsi ya kupambana na tabia ya kununua vitu bila mpangilio wa bajeti kwa kina dada na siri ya urembo toka kwa masuperstaa wa Afrika wanaotikisa ulimwengu wa ulimbwende duniani. Peruzi katika kurasa za jarida la Shear Hair & Beauty ujue mitindo mipya ya nywele, utunzaji wa kucha na mengineo mengi yanayogusa maisha ya mwanamke. Linapatikana kwa wauzaji wote wa magazeti jirani na eneo lako kwa TSh.5,000 tu!
0 comments:
Post a Comment