ANAHITAJI USHAURI

habari dada Shamimu, pole na swaumu.
Nimeona una wasaidia wengi kupitia blog yako upande wa urembo.
Dada nilikuwa naomba unisaidie kuweka hili tatizo watu wanishauri.Ni hivi dada uso wangu     umekuwa hauvutii tena,
nimepoteza rangi yangu ya asili. Naomba niwe mkweli kwenu, anayeniponda aponde atajiju.. unajua. Nimekuwa nikitumia
cream kali ambazo naona ndio chanzo cha kuharibu uso wangu. Nimewahi kupaka aina mbalili mbali za cream hizi nikiziorozesha
zitajaa page ila baadhi ni movate, diproson, betazol n.k. sasa wanajamvi natamani sana kuacha kutumia huo mkorogoo,kwani naona
uso wangu juu ya mashavu kunakuwa kwekundu, je nifanyeje niachapo nispate mazara san usoni, ingawa nina wiki 2 sasa najaribu kupunguza speed
ya kupaka ambapo napaka fair and lovely, na mwili napaka dove moist. lotion. Nimekoma kupka hizi cream kali jamani ila sitaki kuacha watu wakanishangaa, shamimu mambo ya kuiga mabaya, wanawake wenzangu madortor wa ngozi nishaurini lengo niwe na ngozi yenye afya na mzuri, je kitu gani naweza paka nikawa mzuri tu, ngozi yangu ni ya mafuta wadau, basi huku ughaibuni ukipita wazungu wanakushangaa mpaka naona aibu
na summer hii lakini bado nafunga skafu kweni hata upande wa shingoni kwekundu,kuna waafrica wanatuletea haya mavitu huku.

0 comments:

Post a Comment