SHUKRAN

SHUKRANI

Familia ya Bi Rehema Jema Lugome wa Yombo Vituka Dar es Salaam, inatoa shukrani za pekee kwa ndugu, jamaa na marafiki wote walioshiriki nasi kipindi chote cha kumuuguza mgonjwa.

Pia Familia inatoa shukrani za dhati kwa kutufariji wakati wa msiba wa mpendwa wetu JUMA CHINAVACHI aliyefariki tarehe 02/07/2010 na kuzikwa kijijini kwao Nanyamba – Mtwara tarehe 04/07/2010.

Tunawashukuru kwa faraja zenu wakati wa kipindi chote kigumu cha msiba.  Tunawaomba wote kwa pamoja mzipokee shukrani zetu kwa njia hii maana hatuna njia rahisi ya kumfikia kila mmoja.

Familia inapenda kuwajulisha kuwa kutakuwa na Arobaini na Kisomo cha kumuombea marehemu tarehe 06/08/2010 kuamkia tarehe 07/08/2010 nyumbani Yombo Vituka.  Wote mnakaribishwa!

Kwa maelekezo zaidi wasiliana na:-
Fina  Kung’s   0715 302666
Sophia (Mama P) 0784 214545


Inna Lilah Wahina Lilah La’Ajuhun!

Wabilah Tawfiq  Amina!

0 comments:

Post a Comment